COVID-19 na Wafanyakazi Bilioni Mbili Duniani wa Uchumi Usio Rasmi

Group of informal economy workers, all women

Jukwaa la mshikamano wa kimataifa la Mtandao wa WIEGO 

Mei 1, 2020

English   Español   Français   Hindi   Kiswahili   русский


Sisi shirika za wafanyakazi wa uchumi usio rasmi ulimwenguni kote zinaomba serikali zote katika ngazi zote, waungane nasi katika juhudi za kusaidia, kuokoa na kustahimili zinazotokea ngazi ya chini wakati huu wa misiba isiyokuwa ya kawaida.

Wafanyakazi wa uchumi usio rasmi wapo - na tangu siku zote huwa Wafanyakazi muhimu

Wauzaji wa barabarani na wafanyabiashara sokoni ni kiungo muhimu cha usalama wa chakula na mahitaji ya kimsingi, zaidi sana kwa jamii maskini zaidi. Wachambuaji/wasafishaji wa taka pamoja na huduma dhabiti za taka wanachangia katika afya ya umma, kupunguza gharama za tovuti za taka na kuboresha mazingira yenye afya. Wafanyakazi wa ndani wapo kwenye mstari wa mbele kwa kufikia viwango vya usafi na kutoa huduma kwa wagonjwa, wazee na kadhalika. Wafanyakazi wa nyumbani wanahakikisha minyororo ya usambazaji inaendelea sawa na wanashona barakoa na mavazi ya waganga kwa wafanyakazi wa mstari wa mbele. Kila mahali uchumi hutegemea kazi zetu.

Uchumi wa Dunia Hauwezi Kupona Bila sisi

Kusithishwa shughuli za kawaida na harakati zingine za kuzuia COVID-19 zinaathiri vibaya 81% (asilimia 81) ya wafanyakazi bilioni 3.3 ulimwenguni, kama linavyosema Shirika la Kazi la Kimataifa. 61% (asilimia 61) ya hao wafanyakazi wa ulimwengu wote yaani wafanyakazi zaidi ya bilioni mbili - hawaajiriwi rasmi. Katika nchi zinazoendelea idadi yetu ni 90% (aslili mia 90) ya jumla ya wafanya kazi.

Hatua za afya za umma ambazo zinazuia shughuli mbalimbali za watu zimezuia wanachama wetu wengi kufanya kazi zao kabisa. Kila siku ambayo hawatumiki, hawawezi kupata chochote. Wakiikaa nyumbani watakufa na njaa na hawawezi kufanya kazi bila kujiweka wazi kwa maambukizi ya virusi hivi. Misaada inayotolewa katika nchi nyingi haiwafikii wafanyakazi wetu. Kufukuzwa kwa kikatili na dhuluma ya nyumbani zidi ya wanawake inasambaa. Utafiti wetu juu ya matokeo ya mwanzo ya janga hili unaonyesha kwamba mapato katika sekta zetu yameathiriwa sana. Wafanyakazi katika uchumi usio rasmi ambao kwa mda mrefu tu hawana kinga ya kijamii na ambao wanakuwa na ukosefu wa huduma za afya wanakabiliwa na matokeo mabaya sana. Jamii zinahitaji mashirika ya wafanyakazi wa uchumi usio rasmi 'kusaidia kubuni sera madhubuti za umma kujibu shida hii, na kuwa na mtazamo wa kuponya uchumi na kurekebisha muundo.

Lazima Uchumi Uundwe kupya ili uambatane na kanuni za msingi za ujumuishaji

Janga hili la COVID-19 limevutia umakini wa ulimwengu kwa ukosefu wa usawa wa mda mrefu kufuatana na namna ambayo serikali na viwanda hushughulika na wafanyakazi wasio rasmi wa ulimwengu ambao ni wengi sana. Shirikisho la Kimataiaf la Wafanyakazi wa ndani (International Domestic Workers’ Federation), StreetNet International, HomeNet Asia Kusini, HomeNet Kusini mashariki mwa Asia, HomeNet Mashariki ya Ulaya na Asia ya Kati, na Jumuiya ya Kimataifa ya Wachaguaji wa Taka (Global Alliance of Waste Pickers) - kama wanamemba wa Mtandao wa WIEGO - wanahimiza watunga sera kutekeleza kanuni zifuatazo katika huduma zao zote. misaada ya dharura na uokoaji, na katika mikakati yao ya kusimamia afya ya umma na shughuli za kiuchumi:

  1. HAKUNA CHOCHOTE KWETU BILA SISI. Sisi, harakati za kimataifa za wafanyakazi katika uchumi usio rasmi, tunao uzoefu wa miongo kadhaa katika kuandaa na kuwezesha uhusiano kati ya wafanyakazi, jamii, serikali na viwanda. Viongozi wetu ni wenye uzowefu na ujuzi, na ni waelimishaji wenye sifa nzuri, wanajua utendaji takika sekta zao, na wanafanya kazi kwa bidii wakishughulikia janga kubwa hili linalowakabili washiriki wetu wa chini na kudumisha mshikamano wa kijamii katika mazingira ya janga. Kutujumuisha sisi katika utoaji wa maamuzi utafaidisha sio tu wale 61% ya wafanyakazi wa ulimwengu ambao hawakuajiriwa rasmi, lakini pia jamii za mitaa, uchumi wa kitaifa na mifumo ya kimataifa ambayo inatuunganisha sote.
     
  2. USIDHURU. Sera na mazoea za wakati na baada ya janga la COVID-19 lazima ziwatambue wafanyakazi katika uchumi usio rasmi na mashirika yao, na watoe maagizo ya wazi kwa maafisa wa kutekeleza sheria kukataa unyanyasaji, dhuluma, rushwa, kufukuzwa kwa kulazimishwa, na ubomoaji wa mali za wafanyakazi, pamoja na nyumba zao na maeneo yao ya kazi. Inabidi kuweka makini zaidi kwa hatari na gharama zinazochukuliwa na wafanyakazi wa wanawake katika hali ya sasa na kwa muda mrefu.
     
  3. TAZAMA MABADILIKO. Kuna haja ya mtindo mpya wa kazi na uzalishaji, usawa na ugawaji, unaotambua na kuthamini aina zote za kazi. Mabadiliko yanayohitajika ili kufikia mtindo huo yanapashwa kuanza sasa hivi, pamoja na kujitolea kwa mipango ya uokoaji ambayo inazingatia mabadiliko kutoka kwa uchumi usiyo rasmi kwenda kwa uchumi rasmi sambamba na Pendekezo 204 la Shirika la Kazi la Kimataifa. Uwekezaji wa muda mrefu unahitajika ili kujenga tena uchumi duniani unaoambatana na kuelewa kwamba wafanyakazi wa uchumi usio rasmi, ikiwa ni pamoja na wanawake, kuendeleza familia, jamii, na uchumi; ni msingi kwa ujenzi wa minyororo ya thamani ya jamii; na kuhitaji dhamana ya viwango bora vya kazi katika sekta zote.

Shirika zilizosaini hapo chini ni wanachama wa harakati za wafanyikazi wasio rasmi ulimwenguni zinazoendelea kuongezeka ambao pamoja wanawakilisha zaidi ya wanachama milioni mbili ulimwenguni.


International Domestic Workers’ Federation (IDWF)
Elizabeth Tang, Katibu Mkuu, elizabeth.tang@idwfed.org

StreetNet International

Oksana Abboud, Mratibu wa kimataifa, coordinator@streetnet.org.za

HomeNet South Asia
Janhavi Dave, Mratibu wa kimataifa, janhavi.hnsa@gmail.com

HomeNet Southeast Asia
Suntaree H. Saeng-Ging, Mratibu. ss.sunny@hotmail.com

HomeNet Eastern Europe and Central Asia
Violeta Zlateva, Mwenyekiti,  violetazlateva@gmail.com

HomeNet International Working Group
Janhavi Dave, Mratibu wa kimataifa, janhavi.hnsa@gmail.com

Global Alliance of Waste Pickers
Nohra Padilla, Kiongozi, arbesp@gmail.com

Technical Support
Women in Informal Employment: Globalizing and Organizing (WIEGO) 
Sally Roever, International Coordinator, sally.roever@wiego.org

signatory logos
Informal Economy Topic
Informal Economy Theme
Language