Athari za janga la CORONA katika Sekta isiyo rasmi: Wafanyakazi wa Sekta Isiyo Rasmi Dar es Salaam, Tanzania

By:
WIEGO
Date:

WIEGO.2021.Athari za janga la CORONA katika Sekta isiyo rasmi.Dar es Salaam,Tanzania

 

 

 

Janga la COVID-19 katika Sekta isiyo rasmi ni utafiti unaoongozwa na WIEGO kwa miji 12
unaotathmini athari za janga la COVID-19 kwa vikundi maalum vya wafanyakazi wa sekta isiyo
rasmi na kaya zao. Kwa kutumia dodoso la uchunguzi na mahojiano ya kina, Raundi ya 1 ilitathmini
athari za janga mnamo Aprili 2020 (kipindi cha zuio katika miji mingi) na mnamo Julai 2020 (wakati
utafiti ulifanywa na vizuizi vilipunguzwa katika miji mingi)1 ikilinganishwa na Februari 2020 (kabla ya
COVID-19). Kipindi cha 2 kitakagua athari zinazoendelea dhidi ya ishara za kupona mnamo Machi-
Aprili 2021, ikilinganishwa na kipindi cha kabla ya COVID-19 na Kipindi cha 1. Ripoti hii inawasilisha
muhtasari wa matokeo ya Kipindi cha kwanza cha utafiti Jijini Dar es Salaam, Tanzania. Watafiti jijini
Dar es Salaam walichunguza wafanyakazi wa Majumbani 283 ambao ni wanachama wa chama cha
Wafanyakazi wa Hifadhi, Hoteli, Majumbani, Huduma za Jamii na Ushauri (CHODAWU). Walihoji
pia viongozi wawili wa wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi na watoa taarifa wawili muhimu kutoka kwa
mashirika ya wanachama.


Utafiti hutoa wasifu wa wafanyakazi, unaeleza hali zao za kazi na athari za COVID-19. Wakati Tanzania
haikutekeleza zuio la kutoka ndani, utafiti unaonyesha kuwa hali za wafanyakazi wa majumbani tayari
zilikuwa mbaya hata kabla ya janga la COVID 19.

Occupational group
Language
Publication Type